Hata hivyo Washtakiwa hao hawakufikishwa Mahakamani leo kwa sababu Mshtakiwa wa 4 Freeman Mbowe ni mgonjwa kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Magereza.

DPP ameondoa mashtaka hayo mbele ya Jaji Joachim Tiganga ambaye anasikiliza kesi hiyo namba 16 ya mwaka 2021 ambapo Washtakiwa hao leo walipaswa kuanza kujitetea.