Saturday, 26 August 2017

KUHUSU KIPUSA YA ALIKIBA NA ZILIPENDWA YA DIAMOND PLATNUMZ

Na

Charles James

HALI ya hewa mitandaoni imebadilika kinoma-noma, Wakali wawili wanaomiliki jukwaa la Bongo Fleva wamekichafua ile mbaya.

Mechi ya Liverpool na Arsenal Jumapili hii kama imesahaulika hivi, Pambano la ngumi kati ya Mayweather na MacGregory haliongelewi tena Bongo.

Sababu ni moja tu, Mfalme wa Kariakoo na Simba kutoka pori la Tandale wameamua kutufanya mateka wao kwa Mara nyingine nasi tumetii!

Ni muda kidogo watu wamemiss discussion za Ali Kiba na Diamond, watu walikaa kitambo kweli bila kutambiana.

Kumbuka Bongo Fleva imetekwa na Team mbili tu, Team Ali Kiba na Team Diamond.

Takribani juma zima hili wawili hao wamefanikiwa kuteka mitandao ya kijamii, sio IG, FB hadi Tweeter, kote kumenuka baba'ke.

WAMETUFUNGIA MWEZI

Achana na Stori za Lissu kukamatwa wiki hii, weka kushoto ziara ya Rais Magufuli kwenye kivuko cha Kigamboni na kugonga tano na masela.

Michapo ni battle iliyoibuka kati ya Mond na King Kiba.

Ni kama tulishasahau kwamba washikaji wana 'bifu' lao la kitambo, kabla ya wenyewe kuliibua na kulinukisha kinoma.

Mchongo ulianza baada ya Mond kupita katik remix ya Fresh yake Fid Q huku akitupa direct diss kwa Ali.

Mwana nae hakukaa nyuma akaliamsha dude kwenye Social Nets, matokeo yake Stori zimepamba moto na kila mtu anawaongelea sasa.

Usipate shida sana na mabifu yao, pata shida kutambua akili na muziki wao, nini wanakitaka na wala usiangaike kutafuta Nani bora kumzidi mwenzake.

SEDUCE ME VS ZILIPENDWA

Baada ya majibizano yao Kiba anaachia ngoma yake baada ya kitambo kidogo kupita.

Rekodi inaitwa Seduce me au Kipusa; Aisee bonge la wimbo, Ngoma imetulia ingawa baadhi ya watu wanadiss production eti haijatulia.

Lakini binafsi Ilo sijaliona na sitaki kupata shaka na uwezo wa Man water katika kuproduce ngoma. Mixing na Mastering vyote vimetulia.

Turudi hapa: Kipusa ni ngoma ambayo imekaa katika levo ya Kimataifa zaidi, rhythm, melody na hata beat na snare, haipo Ki-Bongo Fleva.

Ni aina ya muziki ambao wanafanya akina Jadin, Maroon na wakali wengine wa State, haupo hata Nigeria achilia mbali SA.

Rekodi nzuri sana kwa watu wanaojua muziki mzuri ila kwa watu ambao hawakumbuki lini wamesikia ngoma Kali watasema ni mbaya.

Nimemuona Kiba wa tofauti kidogo, ambye amepunguza utundu kwenye uandishi huku akiongeza umafia kwenye style na Voko.

Ali hajawahi kuwa na biashara nzuri ya Video but this time around nimeielewa video ya Kipusa.

Zile ndio video ambazo akina Jason, BIG Sean  na Pharell wanachukuliaga tuzo. Sio lazima video ijae vimwana na madansa wengi ndio Iwe kali.

Nimeona watu wanaidiss kuwa ni mbaya nafikiri ni kwa vile haijakaa Kibongo Fleva zaidi, hii inaonesha Ali hakua analenga soko la ndani Bali la Kimataifa.

Amini nawaambieni Kipusa itawapa majibu bomba.

ZILIPENDWA

Usiku tu baada ya Ali kuachia Kipusa, WCB nao wakaamka na kuachia rekodi Kali ya Zilipendwa.

Ngoma imekaa kibongo fleva zaidi na wala haina ubishi hiyo.

Maudhui ya video, mashairi na melody vinajieleza, nafikiri Wasafi hawakutoa ngoma hiyo kulenga soko la Kimataifa, walilenga ' kukwamisha' Kipusa yake Ali.

Sio sawa hata kidogo kuzipambanisha hizi nyimbo maana aina ya muziki uliopigwa ni tofauti kwa pande zote mbili.

Nachoamini hata target ya kila mmoja ipo tofauti, Seduce Me itapenya Nigeria, SA hadi State. Zilipendwa ni yetu hapa hapa.

JAMAA WANATEGEMEANA KINOMA

Kama ilivyo kwa Messi na Ronaldo kwenye Soka ndivyo Ali na Diamond wanavyotegemeana kwenye Game.

Huamini?

Sikia unadhani Diamond alikua na shida ya kuanzisha bifu tena na Ali? Unafikiri ni kweli alivutiwa na Fresh hadi kuomba apite humo?

Umesahau kuhusu Kimwana Hamisa Mobeto.? Ubuyu ulikua umenoga mitandaoni kuwa  Diamond ndio Baba mtoto wa Hamisa.

Licha ya mshikaji kutumia nguvu kubwa kukanusha, bado wana walishakomalia kuwa yeye ndo Baba.

So akaona Solution ni kutengeneza mchongo wa kutusahaulisha iyo scandal ndio hapo bifu lilipoibuliwa tena.

Watu wake wa mikakati wamefaulu katika hili maana bifu limetrend kinoma na sasa tushaanza kusahaulishwa kuhusu mtoto ( ingawa baadae tutarudi nae hahaha)

Ali Kiba nae hakuwa nyuma kunufaika na Mond jamaa alivyojifanya kulianzisha tu nae akatake advantage akajibu mapigo.

Matokeo yake wimbo wake umepata mapokeo makubwa.

I love Diamond, Nampenda Ali Kiba. Siku wakipotea ndio tutajua thamani yao.

No comments:

Post a Comment